• HABARI MPYA

  Tuesday, October 11, 2016

  YANGA KUWAKOSA BUSUNGU NA BOSSOU KESHO MECHINNA MTIBWA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC itawakosa beki wake, Vincent Bossou na mshambuliaji Malimi Busungu katika mchezo wake wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar.
  Yanga itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar kesho Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na wawili hao hawatakuwepo kwa sababu mbalimbali.
  Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba, Bossou hatakuwepo kwa sababu amechelewa kurejea nchini baada ya kwenda kuitumikia timu yake ya taifa, Togo wakati mzalendo Busungu ana matatizo ya kifamilia.
  Bossou hatakuwepo kwa sababu amechelewa kurejea nchini baada ya kwenda kuitumikia timu yake ya taifa, Togo

  Bossou mwenye asili ya Ivory Coast, alikuwa nyumbani jana kuichezea Togo mechi ya kirafiki ikishinda 2-0 dhidi ya Msumbiji Uwanja wa Kegue mjini Lome.
  Mabingwa watetezi, Yanga wameambulia pointi 11 kati ya 18 za mechi sita za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Yanga SC imetoa sare mbili, imefungwa mechi moja na kushinda tatu tangu kuanza kwa Ligi Kuu – hiyo ikiwa ni mbali na kupoteza mchezo wa Ngao ya Jamii mbele ya Azam kwa penalti 4-1 baada ya sare ya 2-2.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA KUWAKOSA BUSUNGU NA BOSSOU KESHO MECHINNA MTIBWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top