• HABARI MPYA

  Thursday, October 13, 2016

  TAMBWE YUKO FITI KUIVAA AZAM JUMAPILI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI tegemeo la mabao la Yanga SC, Amissi Tambwe anatarajiwa kuendelea na mazoezi kesho kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Jumapili.
  Mpachika mabao huyo wa Burundi, aliumia dakika ya 87 jana baada ya kugongana na kiungo wa Mtibwa Sugar, Shaaban Nditi na kupasuka juu ya jicho, hivyo kushindwa kuendelea na mchezo.
  Hata hivyo, Yanga iliyokuwa imemaliza nafasi za kubadilisha wachezaji, ilimalizia pungufu na kufanikiwa kuulinda ushindi wa 3-1.
  Amissi Tambwe anatarajiwa kuendelea na mazoezi kesho kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Jumapili

  Lakini Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba kinara huyo wa mabao wa wana Jangwani hao anaendelea vizuri na kesho ataanza mazoezi.
  Yanga sasa inaelekeza nguvu zake kwenye maandalizi ya mchezo ujao baada ya ushindi wa 3-1 jana mbele ya Mtibwa. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAMBWE YUKO FITI KUIVAA AZAM JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top