• HABARI MPYA

    Monday, October 10, 2016

    SIMBA SC WAOMBA MGAWO WAO MECHI NA YANGA, MADENI BAADAYE

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Simba SC imeomba ipatiwe mgawo wake kamili wa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC iliyofanyika Oktoba 1, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Simba SC haitaki kukatwa fedha za kufidia gharama za uharibifu uliofanywa na mashabiki wake siku hiyo na badala yake imesema italipa deni hilo watakapopelekwa ripoti rasmi.
    Ofisa wa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema jana mjini Dar es Salaam akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE kwamba katika barua yao, Simba wameomba walipwe fedha kamili na deni na faini zozote watalipa baadaye.
    Lakini Mapunda alisema kwamba hawezi kulijibia hilo kwa kuwa lipo nje ya uwezo wake, lakini wanataraji siku mbili hizi watakuwa na majibu bada ya Serikali kutoa msimamo wake.
    “Wenye mamlaka ya kukata au kutokana ni Serikali pekee. Hivyo tusubiri kuona kama atakuwa tayari kulijibia hilo tuma Whindi 
    Serikali imeifungia Simba na watani wao wa jadi, Yanga kutumia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya vurugu za Oktoba 1, mwaka katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacopm Tanzania Bara.
    Vurgu hizo zilifuatia Yanga kupata bao la kuongoza lililofungwa na mshambuliaji Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe dakika ya 26, akimalizia pasi ndefu ya beki Mbuyu Twite na kugeuka mbele ya beki wa Simba, Novat Lufunga kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Vincent Angban.
    Bao hilo lilizua kizaazaa, wachezaji wa Simba wakimvaa refa Martin Saanya wakidai mfungaji, Tambwe aliushika mpira kabla ya kufunga. Na katika vurugu hizo, Saanya alimtoa kwa kadi nyekundu Nahodha wa Simba SC, Jonas Mkude dakika ya 29 kwa sababu ndiye aliyekuwa mstari wa mbele.
    Kwa hali hiyo, mchezo ukasimama kwa takriban dakika tano baada ya mashabiki wa Simba kuanza kufanya vurugu waking’oa viti na kutupa uwanjani. Polisi walitumia milipuko ya gesi za kutoa machozi kuwatuliza mashabiki hao na mchezo ukaendelea hadi Simba SC wakasawazisha dakika ya 87 kwa bao la Shizza Kichuya.
    Tayari TFF imeipiga faini ya Sh. Milioni 5 Simba SC kutoaka na uharibifu huo, wakati Serikali imesema italazimika kulipa uharibu wote uliofanywa na mashabiki wake. 
    Kaimu Mkurugenzi wa Michezo, Alex Nkenyenge alisema kwamba zaidi ya viti 1781 kila kimoja kikiwa na thamani ya Sh. 220,000 vilivunjwa Oktoba 1 katika mchezo ambao uliingiza Sh. Milioni 350 katika viingilio vya mashabiki waliingia kwa tiketi za Elektroniki.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC WAOMBA MGAWO WAO MECHI NA YANGA, MADENI BAADAYE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top