• HABARI MPYA

  Friday, October 07, 2016

  SIMBA SC WAIFUATA MBEYA CITY KESHO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIKOSI kamili cha Simba SC kinaondoka kesho kwenda Mbeya kwa ajili ya mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wiki ijayo.
  Haji Manara, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE jaan kwamba timu inakwenda moja kwa moja Mbeya kesho kwa ajili ya mchezo huo.
  Vinara hao wa Ligi Kuu, Simba SC watakuwa wageni wa Mbeya City FC Jumatano ijayo Uwanja wa Sokono katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. 
  Kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog anatarajiwa kubeba kikosi chake kizima kwenda Mbeya kwa ajili ya mchezo huo, unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua katikati ya wiki.
  Kikosi hicho ni makipa; Vincent Angban, Peter Manyika na Dennis Richard, mabeki; Hamad Juma, Emmanuel Semwanza, Malika Ndeule, Abdi Banda, Juuko Murshid, Janvier Besala Bokungu, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Novart Lufunga na Method Mwanjali. 
  Viungo; Said Ndemla, Mohammed Ibrahim, Awadh Juma, Jamal Mnyate, Jonas Mkude, Shizza Kichuya, Mwinyi Kazimoto na Muzamil Yassin na washambuliaji; Ame Ally, Hajji Ugando, Laudit Mavugo, Frederick Blagnon na Ibrahim Hajib. 
  Mbali na kocha Omog katika benchi la Ufundi wengine ni Msaidizi wake, Mganda Jacksaon Mayanja, kocha wa Makipa; Adam Abdallah, Meneja; Mussa Hassan Mgosi, Mtunza Vifaa; Hamisi Mtambo, Daktari; Yassin Gembe na Mchua Misuli; Salum Abdallah.
  Simba SC inakwenda kwenye mchezo huo ikitoka kutoa sare ya 1-1 na mahasimu wa jadi, Yanga SC Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Simba SC onaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 17, baada ya kucheza mechi saba, ikitoa sare mbili na kushinda tano, wakati Mbeya City ipo nafasi ya sita kwa pointi zake 11, baada ya kucheza mechi saba pia, ikishinda tatu, sare mbili na kufungwa mbili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAIFUATA MBEYA CITY KESHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top