• HABARI MPYA

  Wednesday, October 12, 2016

  SIMBA RAHA MWE! MBEYA CITY KAFA 2-0 PALE PALE SOKOINE…MAMBO YA KICHUYA NA HAJIB

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  SIMBA SC imejiweka sawa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City jioni ya leo Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Shukrani kwa wafungaji wa mabao hayo Ibrahim Hajib Migomba na Shizza Ramadhan Kichuya, wote kipindi cha kwanza na sasa Wekundu wa Msimbazi wanafikisha pointi 20 baada ya mechi nane.
  Kichuya akishangilia baada ya kufunga bao la pili leo Uwanja wa Sokoine

  Hajib alianza kuifungia Simba SC dakika ya sita baada ya shuti lake la mpira wa adhabu kufuatianKichuya kuangushwa kumshinda mlinda mlango kutoka Malawi, Owen Chioma. mpira wa faulo ukapita moja kwa moja wavuni, faulo ilitokana na Kichuya kuangushwa
  Kichuya mwenyewe akafunga bao la pili dakika ya 37 baada ya kuambaa na mpira wingi ya kushoto na kwenda kumtungua Chioma.
  Simba SC ingemaliza kipindi cha kwanza ina mabao zaidi ya mawili kama Muivory Coast, Frederick Blagnom kupoteza nafasi za wazi ikiwemo penalti dakika ya 15 kufuatia yeye mwenyewe kuangushwa, lakini mkwaju wake ulipanguliwa na kipa Chaima.
  Kikosi cha Simba kilikuwa; Vincent Agban, Janvier Bukungu, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Method Mwanjali, Novart Lufunga, Mkude Jonas, Muzamil Yassin, Kazimoto Mwinyi Kichuya/Mohamed Ibrahim dk68, Shiza Kichuya, Frederick Blagnon/Ame Ally dk58 na Ibrahim Hajib/Said Ndemla dk68.
  Mbeya City; Owen Chaima, John Kabanda, Michael Kerenge, Tumba Swedi, Rajab Zahir, Sankhani M, Joseph Mahundi, Kennu Ally, O Ramadhani, Raphael Daudi na Ditram Nchimbi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA RAHA MWE! MBEYA CITY KAFA 2-0 PALE PALE SOKOINE…MAMBO YA KICHUYA NA HAJIB Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top