• HABARI MPYA

  Thursday, October 13, 2016

  SIMBA HATARINI KUMKOSA KICHUYA JUMAMOSI DHIID YA KAGERA SUGAR

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba inaweza kumkosa winga wake, Shizza Ramadhani Kichuya katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumamosi dhidi ya Kagera Sugar.
  Wasiwasi huo unatokana na mchezaji huyo tegemeo la timu kwa sasa kuumia kifundo cha mguu jana, Simba ikishinda 2-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya City Uwanja wa Sokoine.
  Daktari wa Simba SC, Yassin Gembe ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba watalazimika kuisikilizia hali ya Kichuya siku mbili hizi kabla ya kujua hatima yake kuelekea mchezo wa Jumamosi. 
  Shizza Kichuya anaweza kukosekana Jumamosi dhidi ya Kagera Sugar

  Kichuya jana aliseti bao la kwanza lililofungwa na Ibrahim Hajib kabla ya kufunga la pili Simba SC ikijiimarisha kileleni kwa ushindi wa 2-0.
  Hajib alianza kuifungia Simba SC dakika ya sita baada ya shuti lake la mpira wa adhabu kufuatianKichuya kuangushwa kumshinda mlinda mlango kutoka Malawi, Owen Chioma.
  Kichuya mwenyewe akafunga bao la pili dakika ya 37 baada ya kuambaa na mpira wingi ya kushoto na kwenda kumtungua Chioma kwa shuti la mbali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA HATARINI KUMKOSA KICHUYA JUMAMOSI DHIID YA KAGERA SUGAR Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top