• HABARI MPYA

  Saturday, October 15, 2016

  SAMATTA AIOKOA GENK KUZAMA UGENINI UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ametokea benchi na kuisaidia timu yake, KRC Genk kupata sare ya 2-2 na Royal Excel Mouscron katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja Stade Le Canonnier mjini Mouscron.
  Samatta aliingia uwanjani dakika ya 67 kuchukua nafasi ya Mjamaica Leon Bailey na akaenda kumsetia Nikolaos Karelis kufunga bao la pili la kusawazisha dakika ya 78.
  Katika mchezo huo wageni walitangulia kwa mabao ya Mahmoud Hassan 'Trezeguet' dakika ya pili na Valentin Nicolas Viola dakika ya 42, kabla ya Karelis kuifungia la kwanza Genk dakika ya 32.
  Samatta ametokea benchi kuisaidia KRC Genk kupata sare ya 2-2

  Tangu amejiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, Samatta amecheza jumla ya mechi 27 za mashindano yote, 18 msimu uliopita na tisa msimu huu, akifunga mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita.
  Katika mechi hizo, ni 14 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na tatu msimu huu, wakati 12 alitokea benchi nane msimu uliopita na tisa msimu huu – na mechi tisa hakumaliza akitolewa, sita msimu uliopita na tatu msimu huu.
  Kikosi cha KRC Genk leo kilikuwa: Bizot, Walsh/Castagne dk70, Brabec, Colley, Nastic, Ndidi, Pozuelo, Susic/Trossard dk93, Bailey/Samatta dk66, Buffalo na Karelis.
  Mouscron: Delac, Hubert, Markovic/Viola dk35, Trezeguet, Mohamed/Huyghebaert dk85, Diedhiou, Stojanovic/Essikal dk79, Tırpan, Gulan, Peyre na Simic.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AIOKOA GENK KUZAMA UGENINI UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top