• HABARI MPYA

  Friday, October 14, 2016

  PHIRI: SIMBA WANA TIMU YA UBINGWA, ILA YANGA...

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mmalawi wa Mbeya City, Kinnah Phiri ameisifu Simba ni timu nzuri yenye wachezaji wenye uwezo mkubwa, ambao ina nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwishoni mwa msimu.
  Phiri aliyasema hayo jana wakati akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE kwa simu kutoka Mbeya, ambako juzi Mbeya City ilifungwa na Simba SC 2-0 Uwanja wa Sokoine katika mfululizo wa Ligi Kuu.
  Kuhusu kipigo hicho, kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Malawi, alisema kwamba ni bahati mbaya, kwa sababu Mbeya City ilitengeneza nafasi ikashindwa kuzitumia na Simba SC haikufanya makosa kwenye nafasi zao.
  Phiri ameisifu Simba inaweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwishoni mwa msimu

  Lakini pamoja na hayo, Phiri alisema kwamba Simba ni timu nzuri ukilinganisha na timu nyingine za Ligi Kuu msimu huu na anaamini ina uwezo kuchukua ubingwa.
  “Ndiyo, Simba wameuanza msimu huu vizuri sana na wana wachezaji wenye uwezo ukilinganisha na timu nyingine, nawatakia kila la heri watwae ubingwa,”alisema.
  Pamoja na hayo, Phiri alisema kwamba Simba bado wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa mabingwa watetezi, Yanga SC amao wanajivunia silaha ya uzoefu.
  “Niliona mechi ya mahasimu wa jadi (Simba na Yanga). Timu zote ni nzuri na zina wachezaji wenye uzoefu,”alisema Phiri kuhusu mechi hiyo ya Oktoba 1, mwaka huu iliyomalizika kwa sare ya 1-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PHIRI: SIMBA WANA TIMU YA UBINGWA, ILA YANGA... Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top