• HABARI MPYA

  Saturday, October 08, 2016

  PAN AFRICANS KUFANYA UCHAGUZI NOVEMBA 6 DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Pan African inatarajia kufanya mkutano mkuu wa uchaguzi ifikapo Novemba 6 mwaka huu mjini Dar es Salaam.
  Katibu wa Kamati ya Uchaguzi, Peter Mushi  amesema leo kwamba mkutano huo utafanyika kuanzia saa 4:00 asubuhi kwenye Uwanja wa Taifa jijini wanachama wote wenye kadi wanatakiwa kuhudhuriwa huku pia kamati ikialika viongozi mbalimbali wa soka na serikali.
  Shime alisema kuwa katika mkutano huo wanatarajia kupokea ripoti ya mapato na matumizi kutoka kwa viongozi waliomaliza muda wao tangu mwaka 2003 na kufanya mabadiliko ya baadhi ya vipengele vilivyoko kwenye katiba yao.
  "Tunategemea kufanya mabadiliko ya katiba kwa kuondoa cheo cha katibu wa kuchaguliwa na kuwa wakuajiriwa na Mhasibu na msemaji wa klabu," alisema Shime katika taarifa yake.
  Aliongeza kuwa taratibu za mchakato wa uchaguzi huo zitatolewa kuanzia kesho huku pia klabu hiyo imejipanga kuzindua leja mpya yenye majina yote ya wanachama.
  Alisema pia katika mkutano huo wanajipanga kueleza mikakati ya usajili wa wachezaji na ununuzi wa shamba hekari 10 kwa ajili ya kujenga viwanja vitakavyotumiwa na timu za vijana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PAN AFRICANS KUFANYA UCHAGUZI NOVEMBA 6 DAR Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top