• HABARI MPYA

  Sunday, October 09, 2016

  NIGERIA NA MISRI ZASHINDA UGENINI KOMBE LA DUNIA

  TIMU ya taifa ya Nigeria imeanza vizuri mechi za Kundi B kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi baada ya kushinda 2-1 ugenini dhidi ya wenyeji Zambia Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola Jumapili.
  Mabao ya Nigeria yalipatikana kipindi cha kwanza yote yakifungwa na wachezaji wawili wanaocheza England, Alex Iwobi na Kelechi Iheanacho, wakati la Zambia lilifungwa na Collins Mbesuma dakika ya 71.;
  Iwobi aliifungia bao zuri zaidi Super Eagles dakika ya 32 akimtungua kwa shuti kia Kennedy Mweene wa Zambia iliyocheza kwa mara ya kwanza chini ya kocha Wedson Nyirenda .
  Mchezo mwingine, Misri imekwenda kileleni mwa Kundi E kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya Kongo Jumapili  Kintele.
  Manao ya Mafarao yamefungwa na Mohamed Salah na Abdallah Saied wakati la Kongo lilifungwa na Ferebory Dore.
  Timu nyingine katika kundi hilo ni Uganda na Ghana ambazi Ijumaa zilitoka sare ya 0-0 mjni Tamale.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NIGERIA NA MISRI ZASHINDA UGENINI KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top