• HABARI MPYA

  Friday, October 14, 2016

  NGASSA AFUNGUA AKAUNTI YAKE YA MABAO UMANGANI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa leo amefunga bao lake la kwanza katika klabu yake mpya, Fanja ya Oman.
  Ngassa amefunga bao hilo leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Oman, Fanja ikilazimishwa sare ya 1-1 na Al-Nahda Uwanja wa Seeb, Muscat.
  “Nina furaha leo nimefunga bao la kwanza hapa, tena bao zuri tu nikicheza mechi yangu ya pili tu. Namshukuru Mungu, naomba anishikie niendelee kufanya vizuri,”amesema Ngassa akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kwa simu leo kutoka Oman.
  Ngassa (kulia) akiwa na Mtanzania mwenzake wanayecheza naye Fanja, Danny Lyanga 
  ANGALIA VIDEO YA BAO LA KWANZA LA NGASSA OMAN

  Ngassa alijiunga na Fanja mwezi uliopita kwa mkataba wa miaka miwili akitokea ya Free State Stars ya Afrika Kusini.
  Mchezaji huyo wa zamani wa Toto Africans ya Mwanza, Kagera Sugar ya Bukoba, Yanga SC, Azam FC na Simba za Dar es Salaam alijiunga na wawakilishi hao wa Oman kwenye Ligi ya Mabingwa ya Asia, aliondoka Free State mwezi uliopita baada ya kuomba mwenyewe kuvunja Mkataba.
  Ngassa alijiunga na Free State Stars Mei mwaka jana akisajiliwa na kocha Mmalawi, Kinnah Phiri kwa mkataba wa miaka minne.
  Hata hivyo, kocha aliyemsajili baba huyo wa Farida (9) na Faria (7) alifukuzwa baada ya miezi miwili tu na sasa tayari yuko Mbeya City ya Tanzania.
  Katika kipindi cha mwaka mmoja wa kuwa Free State, Ngassa alifanya kazi na makocha wanne akiwemo huyu wa sasa, Mfaransa Denis Lavagne aliyeanza kazi Juni mwaka huu.
  Wengine ni Mjerumani Ernst Middendorp aliyefanya kazi kati ya Septemba na Desemba 2015, Mtaliano Giovanni Solinas aliyefanya kazi kati ya Desemba na Mei 2016.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGASSA AFUNGUA AKAUNTI YAKE YA MABAO UMANGANI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top