• HABARI MPYA

  Thursday, October 13, 2016

  MSUVA: MABAO 50 SI MWISHO WANGU, SAFARI NDIYO KWANZA INAANZA YANGA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  WINGA wa Yanga SC, Simon Happygod Msuva amesema mabao 50 si mwisho wa safari yake ya mafanikio yake kisoka, kwani ana tamaa ya kufika mbali zaidi.
  Msuva alifunga bao lake la 50 jana katiuka mechi 164 tangu ajiunge na Yanga SC mwaka 2012 ikishinda 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Msuva aliyejiunga na Yanga mwaka 2012 akitokea Moro United, jana alifunga bao la pili baada ya Mzambia Obrey Chirwa kufunga la kwanza na baadaye Mzimbabwe, Donald Ngoma akafunga la tatu.
  Simon Msuva amesema mabao 50 si mwisho wa safari yake ya mafanikio yake kisoka
  Simon Msuva (kushoto) akiwa na kiungo Thabani Kamusoko 

  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE  leo, Msuva alisema kwamba mabao 50 si mwisho wa safari yake kwa sababu anataka kufika mbali zaidi.     
  “Ninawashukuru sana wapenzi wa soka nchini, kwani sisi bila ya wao hatuwezi kufika, naushukuru uongozi mzima wa Yanga hadi benchi la ufundi na wachezaji wenzangu pia, maana bila ya wao mimi nisingekuwa hapa nilipo,”alisema.  
  Msuva amesema siri ya mafanikio yake ni jitihada bila kukata tamaa pamoja na nidhamu na kujituma. “Nashukuru vyombo vya habari pia kusapoti soka yetu,”amesema.
  Yanga ilizinduka jana baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu.
  Ushindi huo wa kwanza ndani ya mechi tatu ikitoka kufungwa 1-0 na Stand United na kulazimishwa sare ya 1-1 na mahasimu Simba SC umerejesha matumaini kwa mabingwa hao watetezi. 
  Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 14 baada ya kucheza mechi saba, inazidiwa pointi sita na mahasimu wao wa jadi, Simba SC walio kileleni ingawa wamecheza mechi moja zaidi. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA: MABAO 50 SI MWISHO WANGU, SAFARI NDIYO KWANZA INAANZA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top