• HABARI MPYA

    Sunday, October 09, 2016

    MBEYA CITY WAWACHIMBA KWARA SIMBA SC

    Na Mwandishi Wetu, MBEYA
    BAADA ya mapumziko ya siku moja, kikosi cha Mbeya City FC leo kimeanza rasmi mazoezi kujiweka sawa tayari kwa mchezo mwingine wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Simba  SC  uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine  jumatano ijayo hii  ikiwani siku tano tu baada ya suluhu ya bila kufungana na Stand United.
    Ofisa Habari wa Mbeya City, Dismas Ten amesema kwamba nyota kadhaa waliokosa michezo miwili iliyopita kutokana na majeraha  wamekuwa sehemu ya kikosi kilichofanya mazoezi asubuhi ya leo tayari kwa kuivaa  Simba  Sc siku ya jumatano.
    “Haruna Shamte na Sankhani Mkandawile wamekuwa sehemu ya kikosi kilichofanya mazoezi leo asubuhi, hii ni tafsiri kuwa kikosi chetu kimetimia,Simba ni timu ambayo tunaijua, hatuna shaka nao mara kadhaa wamekuja hapa wakapata kipigo, tunafahamu wamekuwa na mwanzo mzuri wa msimu lakini kucheza na City  ni jambo tofauti inawalazimu kujipanga sana, waje nasisi tupo tayari” alisema.
    Alisema kwamba kikosi chake  kilicheza vizuri  mchezo uliopita dhidi ya Stand United na kufanikiwa kutawala mchezo wa dakika zote, lakini safu ya ushambuliaji haikuwa na baati licha ya kujaribu mara kadhaa kupiga mashuti yaligonga mwamba.
    “Tulikuwa na mchezo mzuri dhidi ya Stand, kwenye soka wakati mwingine bahati huwa ina nafasi yake, Simba wajiandae vya kutoasha kwa sababu  tumedhamiria kufunga magoli mengi,tunajua tabia zao wanapofungwa lakini uwanja wa Sokoine una sura nyingine, jambo muhimu kwa waamuzi tunaomba wachezeshe mchezo kwa kufuata  sheria  17, ili mashabiki wapate burudani na kufurahia ushindi kwa timu yao”, alimaliza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY WAWACHIMBA KWARA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top