• HABARI MPYA

  Saturday, October 15, 2016

  MAVUGO AANZA KUZOESHWA MAISHA YA BENCHI SIMBA

  KWA mara ya pili mfululizo, kocha Mcameroon Joseph Marius Omog hajampanga mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo.
  Simba SC inawakaribisha Kagera Sugar ya Bukoba katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kama ilivyokuwa Jumatano kwenye mechi na Mbeya City, Mavugo na leo yupo benchi.
  Laudit Mavugo ameanzishwa benchi na leo Simba ikimenyana na Kagera Sugar

  Kikosi kinachoanza Simba leo ni; Vincent Angban, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Juuko Murshid, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Muzamil Yassin, Mwinyi Kazimoto, Frederic Blagnon, Ibrahim Hajibu na Shizza Kichuya. 
  Katike benchi wapo Peter Manyika, Abdi Banda, Jamal Mnyate, Mavugo, Novart Lufunga, Said Ndemla na Mohamed 'MO' Ibrahim.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAVUGO AANZA KUZOESHWA MAISHA YA BENCHI SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top