• HABARI MPYA

  Sunday, October 16, 2016

  MAMELODI MKONO MMOJA KWENYE NDOO YA LIGI YA MABINGWA

  MAMELODI Sundown imeweka mkono mmoja kwenye Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Zamalek ya Misri jioni ya leo katika fainali ya kwanza ya michuano hiyo Uwanja wa Lucas Moripe mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
  Shkurani kwa wafungaji wa mabao ya leo, mshambuliaji Mliberia Anthony Laffor dakika ya 31 akimalizia pasi ya kiungo Hlompho Alpheus Kekana, beki Tebogo Langerman dakika ya 40 akimalizia pasi ya mshambuliaji Mzimbabwe Khama Billiat na Islam Gamal aliyejifunga dakika ya 46.
  Mamelodi sasa watahitaji kwenda kuulinda ushindi huo kwa kutokubali kufungwa zaidi ya 2-0 kwenye mchezo wa marudiano Ijumaa ya Oktoba 21, mwaka huu mjini Cairo, Misri ili kutawazwa mabingwa wapya wa Afrika.
  Zamalek iliingia Fainali baada ya kuitoa Wydad Casablanca kwa jumla ya mabao 6-5, wakishinda 4-0 nyumbani Cairo na kufungwa 5-2 ugenini Casablanca. 
  Mamelodi iliitoa Zesco United kwa jumla ya mabao 3-2 ikishinda 2-0 nyumbani baada ya kufungwa 2-1 Zambia.
  Mabingwa wa Afrika msimu uliopita, TP Mazembe ya DRC mwaka huu hawakufuzu hatua ya makundi baada ya kuangukia kwenye Kombe la Shirikisho.
  Hata hivyo, katika michuano hiyo midogo ya klabu barani, Mazembe imefanikiwa kufika fainali ambako itamenyana na MO Bejaia ya Algeria Oktoba 29 katika kabla ya kurudiana Novemba 6, mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAMELODI MKONO MMOJA KWENYE NDOO YA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top