• HABARI MPYA

  Thursday, October 06, 2016

  KIMBEMBE KESHO MBEYA CITY NA STAND UNITED SOKOINE

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  KIKOSI cha  Mbeya FC  kinatarajiwa kushuka kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya kesho kumenyana na Stand United katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Ofisa  Habari wa Mbeya City, Dismas Ten amesema kwamba katika mchezo wa kesho timu yake itawakosa wachezaji wake kadhaa wa safu ya ulinzi kama bekin wa kulia, Haruna Shamte na Sankhani Mkandawile ambao waliumia  kwenye mchezo wa ugenini dhidi ya JKT Ruvu, Mlandizi mkoani Pwani na City wakifungwa bao 2-0.
  “Kwenye kikosi  tunaendelea  kuwakosa Haruna na Sankhani, hii  ni kwa sababu bado wanauguza majeraha lakini taaraiafa njema ni kuwa mlinzi Rajab Zahir amerejea kikosini kuongeza nguvu baaada ya kushindwa kumaliza dakika 90 za chezo dhidi ya Mwadui kufutia maumivu ya kifungo cha mguu, madaktari wamethibitisha kuwa yuko safi na tayari kwa mchezo wa kesho”alisema.
  Nahodha wa Mbeya City FC, Kenny Ally ataiongoza timu yake dhidi ya Stand United kesho

  Katika hatua nyingine, Nahodha wa Mbeya City FC , Kenny Ally ameipogeza timu ya taifa ya vijana Serengeti Boys kwa hatua nzuri waliyofikia licha ya kushindwa kufuzu kwa michuano ya Afrika baada ya kufungwa bao la dakika za lala salama  kwenye mchezo wao wa mwisho huko nchini Kongo - Brazzaville.
  “Kifupi nawapongeza wamefanya kazi kubwa sana, hatua waliyofikia ni ya kujivunia kwa sababu wametegeza mwanga mzuri kwenye mashindan mengine yatakayokuja, hii ni tafasiri kuwa shirikisho letu lilikuwa na  nia ya dhati ya kuhaikisha tunafanikiwa kilichotokea ni sehemu ya mchezo wa soka” alisema.
  Kenny Ally ambaye alikuwa mmoja wa nyota wa timu ya taifa ya Tanzania waliokwenda nchini Brazil na kutwaa kombe la Copa Coca cola licha ya kutoa pongezi wa shirikisho pia alitoa wito kwa rais Jamal Malinzi kuhakikisha anaitunza vyema timu hii ili ije kuwa timu nzuri ya taifa siku za usoni.
  “Nampongeza rais na pia ninatoa wito, kuhakikisha wanaitunza vyema timu hii ili ije kuwa timu bora ya taifa siku zijazo, nakumbuka hali iliyotokea kwetu sisi tuliyoenda Brazil na timu ya vijana wakati huo, baada ya kurudi na kombe, hakuna jambo lolote lililoendelea matokeo yake timu ile ikafa na wachezaji tuliokuwepo kusambaa hovyo hivi sasa kuna ambao wameshaacha soka na wachache tumebaki tunaendelea kucheza”‘ alimaliza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIMBEMBE KESHO MBEYA CITY NA STAND UNITED SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top