• HABARI MPYA

  Tuesday, October 18, 2016

  KICHUYA MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU SEPTEMBA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  WINGA wa Simba SC, Shizza Ramadhani Kichuya amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mwezi Septemba mwaka huu, msimu wa 2016/2017.
  Kichuya aliyesajiliwa msimu huu Simba SC kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, ameshinda tuzo hiyo akiwaangusha Adam Kingwande wa Stand United na Omari Mponda wa Ndanda FC.
  Mchezaji huyo aliisadia timu yake kwa mwezi huo kupata pointi zote 12 katika mechi nne ilizocheza, matokeo ambayo yameifanya Simba iendelee kuongoza Ligi hiyo inayoshirikisha timu 16. 
  Kichuya ndiye Mchezaji Bora wa Ligi Kuu mwezi Septemba mwaka huu

  Kichuya amefunga mabao matatu katika mechi mbili kati ya nne ilizocheza timu yake sambamba na kuseti mabao kadhaa yaliyofungwa na wachezaji wenzake.
  Kwa kushinda tuzo hizo ya mwezi, Kichuya atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.
  Na anakuwa mchezaji bora wa pili wa msimu Ligi Kuu, baada ya Nahodha wa Azam FC, John Bocco kukata utepe kwa ushindi wa Agosti.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KICHUYA MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU SEPTEMBA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top