Tovuti Hii hutembelewa na zaidi ya watu 60,000 kila siku, kutangaza biashara yako na www.binzubeiry.co.tz,
Tuma maombi kwa barua pepe 4thebetter@gmail.com.
 • HABARI MPYA

  Saturday, October 15, 2016

  KICHUYA FITI KUWAVAA KAGERA SUGAR LEO TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WINGA tegemeo wa Simba, Shizza Ramadhani Kichuya yuko fiti kuichezea timu yake leo.
  Simba SC leo watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na mfungaji huyo wa bao la kusawazisha dakika za lala salama katika sare ya 1-1 na watani, Yanga Oktoba 1, anaweza kuchezeshwa.
  Kichuya aliumia kifundo cha mguu Jumatano Simba SC ikishinda 2-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya City na kuzua hofu ya labda ataukosa mchezo wa leo – lakini Daktari wa Wekundu hao wa Msimbazi, Yassid Gembe aliiambia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE jana kwamba winga huyo mwenye kasi anaendelea vizuri.
  Kichuya yuko fiti kuwavaa Kagera Sugar leo katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 

  “Kichuya anaendelea vizuri na leo (jana) jioni atafanya mazoezi. Kwa upande wangu mimi kama daktari anaweza kucheza, sasa ni uamuzi wa benchi la Ufundi tu kumpanga au akutompanga kesho (leo),”alisema Gembe.
  Kichuya Jumatano aliseti bao la kwanza lililofungwa na Ibrahim Hajib kabla ya kufunga la pili Simba SC ikijiimarisha kileleni kwa ushindi wa 2-0.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Note: Only a member of this blog may post a comment.

  Item Reviewed: KICHUYA FITI KUWAVAA KAGERA SUGAR LEO TAIFA Rating: 5 Reviewed By: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top