• HABARI MPYA

    Thursday, October 06, 2016

    KAGERA NA TOTO PATACHIMBIKA KESHO KAITABA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Oktoba 7, 2016 kwa michezo miwili ambako Kagera Sugar itaikaribisha Toto Africans kwenye Uwanja Kaitaba mkoani Kagera wakati Stand United itakuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
    Mbali ya mechi hizo za kesho, Jumamosi Oktoba 8, 2016 pia kutakuwa na michezo mitatu ambako Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati African Lyon itaikaribisha Ndanda FC jijini Dar es Salaam huku JKT Ruvu ikiialika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi ulioko mkoani Pwani.
    Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Mexime kesho atakuwa mwenyeji wa Toto Uwanja wa Kaitaba

    Kwa upande wa Ligi Daraja la Kwanza, kundi A Jumamosi Oktoba 8, kutakuwa na mchezo kati ya Pamba ya Mwanza na Polisi Dar kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam es Salaam wakati African Sports itakuwa mwenyeji wa Kiluvya United kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
    Ligi hiyo ya Daraja la Kwanza itaendelea Jumapili Oktoba 9, 2016 kwa mchezo utakaozikutanisha Ashanti United na Friends Rangers; zote za Dar es Salaam. Kadhalika Jumatatu, kutakuwa na mchezo kati ya Mshikamano ya Dar es Salaam na Lipuli ya Iringa. Mchezo huo, pia utafanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
    Kundi B; Jumamosi Oktoba 8, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Kurugenzi ya Iringa na Coastal Union ya Tanga ufakaofanyika huko Mufindi ukifuatiwa na michezo mitatu siku ya Jumapili Oktoba 9 ambayo Mlale itacheza na Majimaji ya Songea huko Uwanja wa Majimaji Njombe Mji itaikaribisha Kemondo wakati KMC itacheza na Mbeya Warriors kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani.
    Kundi C; Jumamosi Oktoba 8, mwaka huu Mvuvumwa ya Kigoma itacheza na Stand United ya Singida wakati Panamo itapambana na Alliance huku Polisi Dodoma itacheza na Polisi Mara wakati Jumapili Rhino ya Tabora itakuwa mwenyeji wa Mgambo JKT ya Tanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAGERA NA TOTO PATACHIMBIKA KESHO KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top