• HABARI MPYA

  Saturday, October 15, 2016

  WERE APAMBANISHWA NA ONYANGO KUWANIA 'TUZO YA SAMATTA'

  MSHAMBULIAJI chipukizi wa Kenya, Jesse Were ameingia kwenye orodha ya wachezaji 26 wanaowanbia tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika, ambayo imeachwa wazi na Mtanzania Mbwana Samatta.
  Samatta alisajiliwa na KRC Genk ya Ligi Kuu ya Ubelgiji baada ya kutwaa tuzo hiyo Januari mwaka huu kufuatia kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na TP Mazembe ya DRC pamoja na kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo.
  Jesse Were anawania tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika 

  Katika orodha hiyo iliyotolewa leo na Shirikisho la Soka Afrika, yumo pia kipa wa Uganda, Dennis Onyango anayedakia Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Itumeleng Khune wa Afrika Kusini na Kaizer Chiefs ya kwao na Aymen Mathlouthi wa Tunisia na Etoile du Sahel ya kwao.
  Wengine ni Joel Kimwaki wa DRC na TP Mazembe, Joyce Lomalisa wa DRC na AS Vita, Salif Coulibaly wa Mali na TP Mazembe, Ali Gabr wa Misri na Zamalek, Keegan Dolly wa Afrika Kusini na Mamelodi Sundowns, Jackson Mwanza wa Zambia na Zesco United na Rainford Kalaba wa Zambia na TP Mazembe.
  Wamo pia Elia Meschak wa DRC na TP Mazembe, Aymen Hefny wa Misri na Zamalek, Morgan Betorangal wa Chad na MO Bejaia, Hlompho Kekana wa Afrika Kusini na Mamelodi Sundowns, Hamza Lahmar wa Tunisia na Etoile du Sahel, Idris Mbombo wa DRC na Zesco United, Chisom Chikatara wa Nigeria na Wydad Casablanca na William Jebor wa Liberia na Wydad Casablanca.
  Wengine ni Reda Hajhouj wa Morocco na Wydad, Fabrice Nguessi Ondama wa Kongo na Wydad, Mfon Udon wa Nigeria na Enyimba, Bassem Morsi wa Misri na Zamalek, Khama Billiat wa Zimbabwe na Mamelodi Sundowns na Yannick Zakri wa Ivory Coast na Mamelodi Sundowns.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WERE APAMBANISHWA NA ONYANGO KUWANIA 'TUZO YA SAMATTA' Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top