• HABARI MPYA

    Tuesday, October 11, 2016

    ITC YA MIDO MPYA MKONGO WA SIMBA IPO NJIANI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limewatuliza Simba SC kuhusu Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya kiungo Mussa Ndusha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), likisema inaweza kuwasili wakati wowote kuanzia sasa.
    Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas Mapunda aliiambia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE jana kwamba wamewasiliana na Shirikisho la Soka DRC kuhusu ITC ya Ndusha na wamesema wanatuma.
    “Yaani sisi tunawasubiri wao tu watume, wamesema wanatuma. Wakati wowote ikitumwa tutawapa Simba leseni waanze kumtumia,”alisema Mapunda.
    ITC Mussa Ndusha (kulia)  inaweza kuwasili wakati wowote kuanzia sasa kwa mujibu wa TFF

    Ndusha ni mchezaji pekee wa kigeni ambaye Simba imemsajili msimu huu, lakini imeshindwa kumtumia kutokana na kuchelewa kwa ITC yake.
    Wachezaji wengine wa kigeni wa Simba SC ni kipa Vincent Angban, mshambuliaji Frederick Blagnon wote raia wa Ivory Coast, mabeki Juuko Murshid kutoka Uganda, Janvier Besala Bokungu kutoka DRC, Method Mwanjali kutoka Zimbabwe na washambuliaji Laudit Mavugo kutoka Burundi.
    Ndusha yumo mjini Mbeya na kikosi cha Simba SC ambako wamekwenda kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mbeya City. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ITC YA MIDO MPYA MKONGO WA SIMBA IPO NJIANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top