• HABARI MPYA

  Saturday, October 15, 2016

  HANS POPPE: KICHUYA AMENIFANYA NISHEREHEKEE VIZURI MIAKA YANGU 60

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe (pichani kushoto) amesema kwamba Shizza Kichuya amemfanya asherehekee vizuri miaka 60 ya kuzaliwa kwake leo.
  Kichuya amekuwa nyota wa mchezo kwa mara nyingine, akiseti bao la kwanza kabla ya kufunga mwenyewe la pili Simba SC ikishinda 2-0 dhidi ya Kagera Sugar katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jioni ya leo.
  Ushindi huo unawafanya vijana wa Joseph Marius Omog, kocha Mcameroon wafikishe pointi 23 baada ya kucheza mechi tisa za Ligi Kuu, wakiendelea kuongoza kwenye msimamo.
  Na Hans Poppe amesema; “Kwa kweli nimefurahi mno, leo ninasherehekea kutimiza miaka 60 nikifurahia kazi nzuri ya Kichuya na wenzake,”. 
  Simba SC ilipata bao lake la kwanza dakika mbili kabla ya mapumziko, mfungaji kiungo Muzamil Yassin aliyemalizia kwa kichwa kona ya winga Kichuya.
  Shizza Kichuya akafunga mwenyewe kwa penalti dakika ya 75 kuipatia Simba bao la pili baada ya beki Juma Ramadhani kumuangusha kwenye boksi Mohammed ‘Mo’ Ibrahim.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HANS POPPE: KICHUYA AMENIFANYA NISHEREHEKEE VIZURI MIAKA YANGU 60 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top