• HABARI MPYA

  Wednesday, October 12, 2016

  HAJIB ANAANZISHWA NA BLAGNON, MAVUGO LEO BENCHI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mcameroon wa Simba SC, Joseph Omog amewaanzisha pamoja washambuliaji mzalendo Ibrahim Hajib na Frederick Blagnon kutoka Ivory Coast katika mchezo dhidi ya Mbeya City jioni ya leo.
  Simba watakuwa wageni wa Mbeya City jioni ya leo Uwanja wa Sokoine, Mbeya katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania na Omog kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa Ligi Kuu anawaanzisha pamoja wawili hao.
  Na hiyo inatokana na Mrundi Laudit Mavugo ambaye amekuwa akichezeshwa pamoja na Hajib kuanzishiwa benchi leo.
  Frederick anaanza leo pamoja na Ibrahim Hajib leo dhidi ya Simba SC

  Kikosi kamili kinachoanza Simba leo ni; Vincent Agban, Janvier Bukungu, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Method Mwanjali, Novart Lufunga, Mkude Jonas, Muzamil Yassin, Kazimoto Mwinyi
  Kichuya, Shiza Kichuya, Frederick Blagnon na Hajib.
  Katkka benchi wapo Peter Manyika Jr, Banda Abdi, Juuko Murshid, Ndemla Said, Ame Ally na Mo ibrahim.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAJIB ANAANZISHWA NA BLAGNON, MAVUGO LEO BENCHI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top