• HABARI MPYA

  Wednesday, October 05, 2016

  GRANT ATAJA KIKOSI CHA KUIVAA UGANDA, TOGO WAIPIGA 1-0 THE CRANES

  KOCHA wa Ghana, Avram Grant ametaja kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mchezo wa Kundi E kufuzu Kombe la Dunia Urusi mwaka 2018 dhidi ya Uganda Ijumaa mjini Tamale.
  Kiungo anayecheza Norway, Gilbert Koomson ameitwa kwa mara ya kwanza wakati kiungo Enoch Adu Kofi, anayecheza Sweden amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kwa mara ya kwanza tanfu Desemba mwaka 2014.
  Nahodha Asamoah Gyan atakiongoza kikois chenye wachezaji wengi wapya ambacho ndani yake, Grant amewaita pia wachezaji wanaocheza Hearts Of oak ya nyumbani, beki Inusah Musah wa Hearts Of Oak na Emmanuel Ocran.
  Kongo watamenyana na Misri katika mchezo mwingine wa Kundi E Jumapili ya Oktoba 9 mjini Kintele.
  Kikosi kamili  cha Ghana kinaundwa na makipa; Razak Braimah (Cordoba, Spain), Adam Kwarasey (Rosenborg, Norway) Richard Ofori (Wa All Stars)
  Mabeki: Harrison Afful (Columbus Crew, USA), Daniel Amartey (Leicester City, England), Jeffery Schlupp (Leicester City, England), Baba Rahman (Schalke, Germany), John Boye (Sivasspor, Turkey), Jonathan Mensah (Anzhi, Russia), Edwin Gyimah (Orlando Pirates, South Africa), Inusah Musah (Hearts of Oak)
  Viungo: Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese, Italy), Afriyie Acquah (Torino, Italy), Thomas Partey (Atletico Madrid, Spain) Enock Adu Kofi (Malmo, Sweden) Samuel Tetteh (Leifering, Austria), Mubarak Wakaso (Panathinaikos, Greece), Frank Acheampong (Anderlecht, Belgium), Christian Atsu (Chelsea, England), Gilbert Koomson (Songdal, Norway), Emmanuel Ocran (Wa All Stars)
  Washambuliaji: Asamoah Gyan (Al Ahli, UAE), Jordan Ayew (Aston Villa, England), Abdul Majeed Waris (Lorient, France), David Accam (Chicago Fire, USA).
  Wakati huo huo: Uganda, The Cranes jana imefungwa 1-0 na wenyeji Togo katika mchezo wa kirafiki mjini Lome. Kenya nayo imeshinda 1-0 ugenini dhidi ya DRC katika mchezo mwingine wa kirafiki wa kimataifa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GRANT ATAJA KIKOSI CHA KUIVAA UGANDA, TOGO WAIPIGA 1-0 THE CRANES Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top