• HABARI MPYA

  Monday, October 17, 2016

  BOSSOU KUREJEA YANGA IKIIVAA TOTO MWANZA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI Mtogo wa Yanga, Vincent Bossou ameanza kufanya mazoezi na timu yake kufuatia kuwa nje kwa wiki moja kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Malaria.
  Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE leo kwamba, Bossou aliyerejea wiki iliyopita kutoka kuichezea timu yake ya taifa, alishindwa kuingia moja kwa moja kwenye programu za timu kutokana na kufika anaumwa Malaria.
  “Alifika hapa siku tano zilizopita akiwa anasumbuliwa na Malaria. Ila kwa sasa anaendelea na amekwishaanza mazoezi,”amesema Hafidh.
  Vincent Bossou hakuwepo wakati Yanga, ikishinda 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar Jumatano na juzi ikilazimishwa sare ya 0-0 na Azam FC Uwanja wa Uhuru

  Bossou hakuwepo katika mechi mbili zilizopita za Yanga, ikishinda 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar Jumatano na juzi ikilazimishwa sare ya 0-0 na Azam FC, zote Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Na sasa beki huyo mwenye asili ya Ivory Coast anatarajiwa kurejea katika mchezo ujao, Yanga ikimenyana na wenyeji, Toto Africans mjini Mwanza Jumatano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BOSSOU KUREJEA YANGA IKIIVAA TOTO MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top