• HABARI MPYA

  Friday, October 14, 2016

  AZAM WAWEKA KAMBI SHINYANGA KUJIANDAA NA YANGA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imeamua kuweka kambi Shinyanga kujiandaa na mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Yanga SC Oktoba 16 mjini Dar es Salaam.
  Uamuzi huo unakuja siku moja baada ya timu hiyo kupoteza mchezo wake dhidi ya wenyeji, Stand United jana Uwanja wa Kambarage, Shinyanga kwa kufungwa 1-0.
  Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi alisema jana katika mazungumzo na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE kwamba timu itabaki Shinyanga kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga Jumapili.
  Azam FC imeweka kambi Shinyanga kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga SC Oktoba 16 

  Alisema kwamba benchi la Ufundi na wahezaji wamekubaliana na matokeo ya jana na sasa wanajipanga kwa mchezo ujao dhidi ya Yanga ili warejeshe heshima.
  “Kwa kweli hali ilivyo inasikitikisha, ila hatujakata tamaa. Tunaendelea kupambana na sasa tunajipanga kwa mchezo ujao,”alisema Iddi.
  Azam FC, washindi wa pili wa msimu uliopita Ligi Kuu – mambo si mazuri msimu huu baada ya kuambulia pointi 11 katika mechi nane, wakishinda tatu, sare mbili na kufungwa mbili hivyo kushika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi. 


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM WAWEKA KAMBI SHINYANGA KUJIANDAA NA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top