• HABARI MPYA

  Saturday, September 17, 2016

  ZAMALEK WAITANDIKA 4-0 WYDAD NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA

  ZAMALEK ya Misri imebisha hodi Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco jana Uwanja wa Borg El Arab katika Nusu Fainali ya kwanza. 
  Mahmoud Abdel-Razek 'Shikabala' alifunga vbao zuri mbele tya mashabiki 85,000 mjini Alexandria baada ya kiungo huyo kukimbia kwa umbali wa mita 56 kabla ya kufumua shuti kali kutoka nje ya boksilililotinga nyavuni.
  Mabao mengine ya Zamalek yalifungwa na Ymen Hefny, Bassem Morsy na Mostafa Fathy aliyetokea benchi kwa penalty .
  Huo ni ushindi wa rekodi katika Nusu Fainali kwa Zamalek, ukiupiku ushindi wa 3-0 nyumbani pia dhidi ya JET (sasa JS Kabylie) ya Algeria mwaka 1984.
  ZESCO United ya Zambia inawakaribisha Mamelodi Sundowns Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola katika Nusu Fainali nyingine.
  Wakati huo huo: Nusu Fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika inachezwa leo, wenyeji Etoile du Sahel wakiikaribisha TP Mazembe ya DRC Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse, Tunisia, wakati kesho Mouloudia Bejaia wataikaribisha FUS Rabat ya Morocco Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia, Algeria. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZAMALEK WAITANDIKA 4-0 WYDAD NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top