• HABARI MPYA

    Thursday, September 15, 2016

    YANGA SC WAWASILI SHINYANGA, ILIBIDI WAPANDE HADI DALA DALA ILI KUWAHI

    Na Mwandishi Wetu, MWANZA
    KIKOSI cha Yanga SC kimewasili salama Shinyanga baada ya safari ya tangu asubuhi kutoka Dar es Salaam kuanzia angani hadi barabarani.
    Yanga walipanda ndege kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza ambako walipanda basi hadi Shinyanga, tayari kwa mchezo wao wa Jumamosi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Hata hivyo, baada ya kufika Mwanza, Yanga walilazimika kukodi Hiece mbili daladala za Uwanja wa Ndege, kwenda Mwanza mjini kupanda basi walilokodi kuwapeleka Shinyanga.
    Basi la Yanga baada ya kuwasili hotelini mjini Shinyanga
    Wachezaji wa Yanga wakiwa ndani ya ndege kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza 
    Kipa Deo Munishi 'Dida' nje ya basi leo wakati wa safari ya Shinyanga
    Hapa wachezaji wa Yanga wanapanda daladala kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza kulifuata basi katikati ya mji kwa safari ya Shinyanga
    Katibu Mkuu wa Yanga; Baraka Deusdedit amesema; “Nachoweza kusema basi lilichelewa kufika Uwanja wa Ndege kuchukua wachezaji, na hatukuona sababu ya kupoteza muda mwingi kulisubiri,”. “Tukaona tuchukue usafiri wowote wa haraka tulifikie kuliko kuwaacha wachezaji wanazagaa ovyo Uwanja wa Ndege, ndiyo tukakodi dala dala,”amesema Deusdedit akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo.  
    Yanga SC watakuwa wenyeji wa Mwadui FC Jumamosi Uwanja wa Kambarage, Shinyanga katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Kwa ujumla Ligi Kuu inaendelea wikiendi hii, mbali ya Yanga na kuwa wageni wa Mwadui Shinyanga – Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Azam FC watamenyana na Simba SC na Mbeya City na Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
    Mtibwa Sugar na Kagera Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro, Ruvu Shooting na Mbao FC Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na Maji Maji na Ndanda FC Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
    Jumapili kutakuwa na michezo miwili, Stand United wakiikaribisha JKT Ruvu Stars Uwanja wa Kambarage, Shinyanga na African Lyon wakimenyana na Toto Africans Uwanja wa Uhuru.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WAWASILI SHINYANGA, ILIBIDI WAPANDE HADI DALA DALA ILI KUWAHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top