• HABARI MPYA

    Sunday, September 04, 2016

    UGANDA WAFUZU KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA BAADA A MIAKA 39

    UGANDA imefuzu Fainali za Mataifa ya Afrika baada ya 39, kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Comoro Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala leo.
    Asante za kutosha kwa mshambuliaji wa Standard Liege ya Ubelgiji, Faruk Miya aliyefunga bao hilo pekee dakika ya akimalizia pasi ya Moses Oloya baada ya shambulizi kalila Cranes.
    Faruk Miya ameifunga bao pekee Uganda akimalizia pasi ya Moses Oloya 

    Kwa ushindi huo, Uganda inamaliza kileleni mwa Kundi D kwa pointi zake 13, ikifuatiwa na Burkina Faso ya pili iliyomaliza na pointi 11, Botswana ya tatu pointi saba na Comoro imeshika mkia kwa pointi zake tatu.
    Mara ya mwisho The Cranes kucheza Afcon ilikuwa mwaka 1978 ilipofanikiwa kufika hadi fainali na kufungwa na Black Stars ya Ghana. 
    Sifa zimuendee kocha Msebia wa The Cranes, Mulitin ‘Micho’ Sredojevic kwa tiketi ya AFCON ya mwakani, baada ya kazi nzuri.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UGANDA WAFUZU KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA BAADA A MIAKA 39 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top