• HABARI MPYA

  Saturday, September 03, 2016

  TAIFA STARS YACHAPWA 1-0, AISHI ADAKA BALAA!

  TANZANIA imehitimisha mechi za Kundi G kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kufungwa bao 1-0 na wenyeji, Nigeria jioni ya leo Uwanja wa Uyo, Akwa Ibom.
  Bao pekee la Super Eagles limefungwa na mshambuliaji wa Manchester City, Kelechi Iheanacho dakika ya 78 katika mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua.  
  Kelechi Iheanacho akishangilia baada ya kufunga bao pekee dakika ya 78 
  Shiza Kichuya (kushoto) na Jonas Mkude (kulia) wa Tanzania wakipambana na wachezaji wa Nigeria

   Stars ingebugizwa mabao mengi leo kama si jitihada za kipa wake, Aishi Manula kuokoa michomo mingi ya hatari.
  Kwa matokeo hayo, Eagles inamaliza nafasi ya pili kwa pointi zake tano, nyuma ya Misri walioongoza kundi na kufuzu AFCON mwakani Gabon, wakati Stars iliyomaliza na pointi moja imeshika mkia.
  Misri iliyovuna pointi 10, imefuzu kiulaimi hususan baada ya Chad kujitoa katika kundi hilo katika ya mechi za kufuzu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YACHAPWA 1-0, AISHI ADAKA BALAA! Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top