• HABARI MPYA

  Saturday, September 03, 2016

  SIMBA YAWATANDIKA 2-0 MAAFANDE WA POLISI DOM

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imewapa raha mashabiki wake baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Dodoma katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
  Shukran kwao wafungaji wa mabao hayo, beki Abdi Banda anayeweza kucheza kama kiungo na kiungo Said Ndemla. 
  Banda aliyesajiliwa msimu uliopita kutoka Coastal Union ya Tanga ndiye aliyeanza kuifungia Simba katika dakika ya 35 akimalizia pasi ya kiungo mkongwe Mwinyi Kazimoto Mwitula.
  Ndemla akafunga bao la pili kwa shuti kali kutoka umbali wa mita 25 dakika ya 63 baada ya kutengeea pasi na Kazimoto aliyecheza vizuri leo Uwanja wa Jamhuri.
  Baada ya mchezo huo, Simba SC iliyo chini ya kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog inatarajiwa kurejea Dar es Salaam kesho kuendelea na maandalizi ya mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Na Simba SC itashuka tena dimbani Jumatano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na Ruvu Shooting ya Pwani katika mfululizo wa ligi hiyo.
  Katika mechi zake mbili za awali za Ligi Kuu, Simba imevuna pointi nne ikishinda 3-1 dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara kabla ya kutoa sare ya 0-0 na JKT Ruvu katika mchezo uliofuata, zote Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
  Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Vincent Angban, Abdi Banda, Malika Ndeule, Novat Lufungo/Emmanuel Semwanza, Method Mwanjali, Said Ndusha, Mwinyi Kazimoto/Mohammed Mussa ‘Kijiko’, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Awadh Juma, Danny Lyanga/Hajji Ugando, Frederick Blaginoni na Said Ndemla.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAWATANDIKA 2-0 MAAFANDE WA POLISI DOM Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top