• HABARI MPYA

  Thursday, September 15, 2016

  SIMBA YAMPIGA BEI UARABUNI STRAIKA WAKE ILIYEMTOA KONGO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imedaiwa kumuuza 'kinyemela' mshambuliaji wake hatari, Danny Lyanga (pichani kulia) kwa klabu ya Oman SC ya Ligi Kuu ya Oman.
  Hata hivyo, Katibu wa Simba, Patrick Kahemele amesema anachofahamu Lyanga amekwenda Oman kwa majaribio na hakuna biashara iliyofanyika hadi sasa.
  Lyanga aliyejiunga na Simba SC msimu uliopita kutoka DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yupo Oman tangu mwezi uliopita.
  Na chanzo kimesema mshambuliaji huyo mwenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira anaendelea vizuri katika klabu hiyo ya Jiji la Muscat.
  Hata hivyo, haijajulikana Lyanga amesaini miaka mingapi na kama Simba SC imemuuza kweli imepewa kiasi gani cha fedha kwenda klabu hiyo ya Oman.
  Lyanga alikuwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake Simba SC na ni kati ya wachezaji ambao huwezi kusita kusema walifanya vizuri msimu uliopita klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAMPIGA BEI UARABUNI STRAIKA WAKE ILIYEMTOA KONGO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top