• HABARI MPYA

    Saturday, September 17, 2016

    SHIZA KICHUYA AING'ARISHA SIMBA, AZAM WAKAA WAZIMAAAA!

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BAO pekee la Shiza Ramadhani Kichuya limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
    Kichuya alifunga bao hilo dakika ya 67 kwa shuti la kitaalamu baada ya kupokea pasi nzuri ya kiungo Said Hamisi Ndemla.
    Kwa ushindi huo, Simba SC sasa inajinafasi kileleni mwa Ligi Kuu, ikifikisha pointi 13 baada ya mechi tano, ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 10 sawa na Azam.

    Shiza Kichuya akishangilia baada ya kuifungia Simba SC bao pekee leo
    Winga Muivory Coast wa Azam FC, Ya Thomas Renardo akiwatoka mabeki wa Simba leo
    Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Hajib akiwatoka mabeki wa Azam FC leo
    Mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco akifumua shuti mbele ya beki wa Simba, Method Mwanjali
    John Bocco akigombea mpira wa juu na beki wa Simba Novaty Lufunga

    Simba SC walistahili ushindi katika mchezo wa leo kutokana na kupeleka mashambulizi mengi zaidi langoni mwa Azam FC.
    Hata hivyo, umaliziaji haukuwa mzuri leo kwa Wekundu wa Msimbazi, kwani walipoteza nafasi kadhaa nzuri za kufunga tangu kipindi cha kwanza.
    Nahodha wa Azam FC, John Bocco aliyekuwa mshambuliaji pekee leo alijitahidi lakini hakuweza kufurukuta mbele ya mabeki wa Simba SC, Novaty Lufunga na Mzimbabwe Method Mwanjali.   
    Ibrahim Hajib alikuwa tishio zaidi kwenye safu ya ulinzi ya Azam FC, lakini hakuweza tu kufunga, wakati Mrundi Laudit Mavugo hakufurukuta kabisa na akatolewa kipindi cha pili Muicory Coast, Frederick Blagnon aliyekwenda kukosa bao la wazi.
    Ushindi huo ni faraja kwa kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog kwani ameifunga timu yake ya zamani, Azam FC iliyomfukuza mwaka jana.
    Kikosi cha Azam FC kilikuwa: Aishi Manula, Shomary Kapombe, Bruce Kangwa, David Mwantika, Jean Baptiste Mugiraneza, Himid Mao, Frank Domayo/Mudathir Yahya dk76, Salum Abubakar ‘Sure Boy’,Ya Thomas Renardo, John Bocco na Khamis Mcha ‘Vialli’/Francesco Zekumbawira dk76.
    Simba: Vincent Angban, Janvier Besala Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, Shiza Kichuya/Mohamed Ibrahim dk, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo/Frederick Blagnon dk, Jonas Mkude, Ibrahim Hajib na Jamal Mnyate/Said Ndemla dk63.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SHIZA KICHUYA AING'ARISHA SIMBA, AZAM WAKAA WAZIMAAAA! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top