• HABARI MPYA

  Sunday, September 04, 2016

  RWANDA YAIKATALIA GHANA, SARE 1-1 ACCRA KUFUZU AFCON

  RWANDA imefanikiwa kupata sare ugenini, baada ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Ghana katika mchezo wa mwisho wa Kundi H kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Uwanja wa Accra Sports mjini Accra, Ghana.
  Pamoja na kulazimishwa sare hiyo, Ghana bado inamaliza kileleni mwa kundi hilo kwa pointi zake 14 kutokana na mechi sita, ikifuatiwa na Msumbiji pointi saba, Rwanda pointi sita sawa na Mauritius.
  Katika mchezo wa jana, Black Stars walitangulia kwa bao la Samuel Tetteh dakika ya 24, kabla ya Muhadjiri Hakizimana kuisawazishia Rwanda dakika ya 83.
  Kwa maatokeo zaidi mechi za kufuzu zaidi AFCON jana waweza kutazama MATOKEO MECHI ZA KUFUZU AFCON JANA  na ratiba ya mechi za leo MECHI ZA LEO KUFUZU AFCON wakati kujua msimamo wa makundi gonga MSIMAMO WA MAKUNDI YOTE KUFUZU AFCON 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RWANDA YAIKATALIA GHANA, SARE 1-1 ACCRA KUFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top