• HABARI MPYA

  Tuesday, September 06, 2016

  MSONDO FAMILY DAY SASA NI ZAMU YA KINONDONI SEPTEMBA 30

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BAADA ya Msondo Ngoma kulingurumisha lile onyesho lao la Msondo Family Day katika wilaya za Temeke na Ilala sasa ni zamu ya wakazi wa Kinondoni.
  Onyesho hilo ambalo hufanywa kila wikiendi ya mwisho wa mwezi, safari hii litafanyika Mango Garden Kinondoni Ijumaa ya Septemba 30.
  Mmoja wa waratibu wa onyesho hilo, Abdulfareed Hussein, ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE kwamba maandalizi ya Msondo Family Day ndani ya Kinondoni tayari yameshika kasi.
  “Kwa kawaida kwetu sisi, linapoisha onyesho moja basi ndiyo mwanzo wa maandalizi ya onyesho linalofuata,” alitamba Abdulfareed.
  Kama ilivyo ada, dhumuni la ‘Msondo Family Day’ ambayo hufanyika kila wikiendi ya mwisho wa mwezi, ni kuongeza mshikamano baina ya wanamuziki wa Msondo, mashabiki na wadau wakubwa wa bendi hiyo.
  Abdulfareed ameongeza kuwa onyesho hilo maalum la kila mwezi, halitaishia Dar es Salaam pekee bali litafika hadi mikoani.
  Mratibu huyo amesema zawadi mbali mbali za papo kwa papo ni sehemu ya Msondo Family Day. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSONDO FAMILY DAY SASA NI ZAMU YA KINONDONI SEPTEMBA 30 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top