• HABARI MPYA

  Thursday, September 15, 2016

  MICHAEL ESSIEN ABISHA HODI LIGI KUU YA AUSTRALIA

  NYOTA wa zamani wa Ghana, Michael Essien yuko mbioni kujiunga na Melbourne Victory ya Ligi Kuu ya Australia, maarufu kama 'A-League'.
  Kwa mujibu wa Herald Sun, Essien atakuwa mchezaji wa pili kusaini chini ya sheria mpya ya Shirikisho la Soka Australia (FFA) juu ya wachezaji wa kigeni, ndani ya mwezi mmoja kabla ya kwanza kwa msimu mpya. 
  Mtendaji Mkuu wa FFA, David Gallop amethibitisha kwamba Essien ameridhishwa na vigezo. 
  “FFA iliombwa na klabu ya A-League kutumia sheria mpya kumleta Michael Essien katika A-League acheze kwa msimu mzima,”alisema.
  Michael Essien yuko mbioni kujiunga na Melbourne Victory ya A-League ya Australia 

  Essien alicheza mechi 168 enzi zake Chelsea ndani ya miaka yake tisa akishinda mataji mawili ya Ligi Kuu, Kombe la FA mara nnee na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ghana pia amechezea AC Milan, Real Madrid na Lyon katika miaka yake 16 ya kucheza Ulaya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MICHAEL ESSIEN ABISHA HODI LIGI KUU YA AUSTRALIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top