• HABARI MPYA

  Friday, September 16, 2016

  MBEYA CITY WATAMBA WAKO TAYARI KWA PRISONS KESHO SOKOINE

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  MBEYA City FC imesema iko tayari kwa mchezo dhidi ya mahasimu wao wa Jiji la Mbeya, Prisons katika Ligi Kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara kesho Uwanja wa Sokoine mjini hapa.
  Ofisa Habari wa Mbeya City, Dismas Ten amesema leo kwamba maandalizi ya kikosi chacke kuelekea mchezo huo yamekamilika na wana matarjio ya kufanya vizuri.
  “Kesho ni siku ya mchezo, kwetu  sisi huu ni mchezo muhimu kwa sababu tunahitaji  kushinda ili tuendelee kuwa kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi, maandalizi ya kutosha yamefanyika kwa hiyo  ni nafasi kwa mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kusapoti timu yao, jopo la madaktari wetu limenithibitishia kuwa  Geoffrey Mlawa hatakuwepo uwanjani hiyo kesho lakini nyota wengine wako kwenye hali nzuri, huu ni msimu ambao  City inarudi kwenye zama  zake” alisema.
  Mbeya City mazoezini jana kujiandaa na mchezo dhidi ya Prisons

  Video:
  Kuhusu utulivu na amani uwanjani kwa mashabiki watakaojitokeza  kushuhudia mchezo huo, Ten alisema kuwa watu wanatakiwa kuzingatia amani kwa sababu mchezo wa soka hukutanisha watu wengi hivyo ni vyema  mashabiki kushangilia timu zao  huku wakiwa kwenye hali nzuri ya amani.
  “Mashabiki  wa  City  wajitokeze kwa wingi, wasiwe na shaka ya utulivu kwa sababu ulinzi  utakuwepo wa kutosha, amani mchezoni ni jambo jema  hivyo kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake  kuhakikisha  tunashangilia timu yetu vizuri katika kuhanikiza ushindi huku tukiwa na wingi wa amani” alimaliza.
  City inakutana na Prison huu ukiwa ni mchezo wa 7 kwenye mfululizo wa mechi za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara huku rekodi zikionyesha kuwa City imepata ushindi mara 2, Prison wakishinda mara 3 na mara 1 timu hizi zikienda  sare, Kiungo Peter Mapunda ndiye mchezaji anashika rekodi ya kufunga bao la kwanza kabisa kwenye mechi zilizokutanisha timu hizi mbili akifunga bao hilo kwenye mchezo wa duru ya kwanza msimu wa 2013/14  kwenye ushindi wa 2-0, misimu itatu iliyopita. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY WATAMBA WAKO TAYARI KWA PRISONS KESHO SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top