• HABARI MPYA

    Sunday, September 04, 2016

    MBEYA CITY WAPANDA KILELENI LIGI KUU BAADA YA KUWALIPUA MBAO FC 4-1 MWANZA

    Na Mwandishi Wetu, MWANZA
    MBEYA City jana imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji, Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
    Kwa ushindi huo, Mbeya City inapanda kileleni mwa Ligi Kuu kwa kufikisha pointi saba baada ya kucheza mechi tatu zote ugenini Kanda ya Ziwa, ikishinda mbili, ukiwemo dhidi ya Toto Africans 1-0 Mwanza na Kagera Sugar 0-0 Shinyanga. 
    Kwenye Mchezo huo ulioanza kwa kasi  timu zote zikishambuliana kwa zamu, wenyeji walikuwa wa kwanza kulifikia lango la City  baada ya Vicent Philipo kufanikiwa kumtoka Haruna Shamte aliyekuwa anacheza beki ya kulia lakini mpira wa krosi wa mchezaji huyo wa Mbao uliishia mikononi mwa kipa Owen Chaima.
    Haruna Shamte (katikati) Rajab Zahir (kushoto) wakishangilia bao la pili lililofungwa na Omary Ramadhani (kulia)

    City ilijibu shambulizi kwenye dakika ya 20 kupitia Ayoub Semtawa  aliyefanikiwa  kuwatoka walinzi wa Mbao Fc lakini mpira aliompenyezea Omary Ramadhani uliokolewa na walinzi wa timu hiyo mwenyeji kabla  ya  Raphael Daud kufanikiwa kuandika bao la kwanza  baada ya kuunganisha mpira  ulikuwa umepigwa na Ayoub Semtawa kwenye dakika ya 28, bao lililodumu kwa dakika 10  baada ya Vicent Philipo kuswazisha  dakika ya  38 na kumaliza kipindi cha kwanza timu zote zikiwa na bao 1-1.
    Kipindi cha pili Kocha Kinnah Phiri alifanya mabadiliko  ya kumtoa alifanya mabadiliko ya kumtoa  Ayoub Semtawa na nafasi yake kuchukuliwa na Ditram Nchimbi  mabadiliko ambayo  yaliongeza  uhai kweny safu ya ushambuliaji kwani dakika chache baadae Omary  Ramadhani aliiandika  bao la pili, bao lilofuataiwa na mabao mengine mawili kutoka kwa Ramadhani Chombo na Raphael Daud waliohitimisha dakika 90  ubao ukisomeka  mabao 4 kwa City na 1 kwa Mbao Fc.
    Mara baada ya mchezo huo kocha wa City  Kinnah Phiri, pamoja na mengine mengi lakini pia  aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizui kwa kufuata Maelekezo na hatimaye  kuibuka na ushindi  huo mnono.
    “Vijana wangu wamecheza  vizuri,  wamefanya kazi kwenye kila tulichokuwa tunakifanyia mazoezi, tulijua Mbao wangekuja na mchezo wa kasi kwa sababu walihitaji sana kushinda hasa baada ya kupoteza mchezo wao uliopita, tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha  kupata pointi saba kwenye michezo yetu mitatu na sasa tunarudi nyumbani kujiandaa na mchzo mwingine”, alisema.
    City  itaondoka Mwanza  alfajiri ya kesho kuelekea jijini Mbeya tayari kwa matayarisho ya mchezo dhidi ya Azam Fc  uliopangwa  kuchezwa  tarehe 10 mwezi huu kwenye uwanja wa Sokoine.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY WAPANDA KILELENI LIGI KUU BAADA YA KUWALIPUA MBAO FC 4-1 MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top