• HABARI MPYA

  Friday, September 02, 2016

  MASHINDANO YA DISKO TEMEKE YAANZA LEO KINGS PALACE CENTRE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Kings Palace Centre ya Keko Magurumbasi, Dar es Salaam imeandaa mashindano ya vikundi vya Disko Manispaa ya Temeka.
  Mkurugenzi wa Kings Palace, klabu kongwe ya burudani Temeke, Robert Mushi ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kwamba mashindano hayo yanaanza leo Kings Palace.
  Mushi amesema mashindno hayo yatashirikisha jumla ya vikundi 12 kutoka vitongoji tofauti Temeke.
  Alivitaja baadhi ya vikundi hivyo kuwa ni Kigamboni Group, Toroli Squad, Noma Sana, Kazi Kazi, Chuma Chuma, Tandika, Ikulu Vegas, Gusa Unase na Five Star.
  Mushi amesema bingwa atajinyaku;ia zawadi ya Sh. 300,000, mshindi wa pili 200,000 na wa tatu 100,000 katika faibaki itakatiofanyia wiki mbii zijazo baada ya hatua za awali.
  “Tumemua kufufua mashindano ya disko ili kuwapa vijana uwanja wa kuonyesha vipaji vyao baada ya muda mrefu wa kunyimwa fursa hiyo, tunaamini tunafungua njia, na wengine watafuata nyayo zetu tena,”alisema Mushi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MASHINDANO YA DISKO TEMEKE YAANZA LEO KINGS PALACE CENTRE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top