• HABARI MPYA

  Sunday, September 18, 2016

  KILIMANJARO QUEENS YAIFUMUA 4-1 UGANDA NA KUTINGA FAINALI CHALLENGE

  Na Mwandishi Wetu, JINJA
  TIMU ya taifa ya Tanzania Bara ya wanawake, Kilimanjaro Queens imeingia fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji, Uganda leo Uwanja wa Ufundi, Njeru mjini Jinja.
  Kili Queens sasa itamenyana na Kenya, ambayo imeifunga 3-2 Ethiopia katika Nusu Fainali nyingine leo. Mabao ya Tanzania Bara leo yamefungwa na Donosia Daniel dakika ya sita, Mwanahamisi Omari 'Gaucho' dakika ya 17, Stumai Abdallah dakika ya 31 na Asha Rashid 'Mwalala'.
  Fainali ya CECAFA Challenge ya kwanza ya wanawake inatarajiwa kufanyika Septemba 20, ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.
   Kikosi cha Tanzania katika mchezo huo 
  Wachezaji wa Uganda (kushoto) na Tanzania (kulia) wakiwania mpira
  Wachezaji wa Tanzania (kushoto) na Uganda (kulia) wakiwania mpira
  Kikosi cha Uganda katika mchezo huo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KILIMANJARO QUEENS YAIFUMUA 4-1 UGANDA NA KUTINGA FAINALI CHALLENGE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top