• HABARI MPYA

  Friday, September 16, 2016

  JULIO: NAWEZA KUWAOGOPA MBAO, LAKINI SI YANGA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema anaweza kuwaogopa Mbao FC, lakini si Yanga SC.
  Julio ameyasema hayo leo katika mazungumzo na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kutoka Shinyanga kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Yanga.
  Mwadui FC watakuwa wenyeji wa mabingwa watetezi, Yanga SC katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kesho Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
  Na Julio amesema kwamba ana matarajio makubwa ya kuwafunga Yanga kesho, kwa sababu ni timu ya kawaida kimchezo licha ya ukongwe wake na zaidi anajivunia morali ya wachezaji wake kuelekea mchezo huo. 
  Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema anaweza kuwaogopa Mbao FC, lakini si Yanga SC.

  “Namshukuru Mungu niko salama, tunaiheshimu Yanga, ni timu kongwe, mabingwa watetezi, lakini ukubwa wa pua si wingi wa kamasi,”amesema Julio akimaanisha ukongwe wa Yanga haumaanishi ubora wa soka.
  Julio amesema kwamba anashukuru wachezaji wake 25 aliowasajili wako vizuri kuelekea mchezo wa kesho na yeyote atakayempanga anaweza kumletea ushindi.
  “Yanga ni timo ya kawaida, naweza kuiogopa Mbao, lakini sio Yanga, ukicheza na Mbao kwa sababu timu ndogo, watajitahidi wakufunge, lakini Yanga watatuona wa kawaida hawatuogopa,” amesema Julio.
  Yanga SC iko Shinyanga tangu jana asubuhi kwa ajili ya mchezo huo, baada ya kushinda mechi mbili na kutoa sare moja katika michezo yake mitatu iliyotangulia na kocha Pluijm amepania kushinda kesho ili kujiweka vizuri katika mbio za ubingwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JULIO: NAWEZA KUWAOGOPA MBAO, LAKINI SI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top