• HABARI MPYA

    Thursday, September 08, 2016

    JOTO KALI LAVURUGA LA LIGA, MECHI KUAHIRISHWA

    MECHI za Ligi Kuu ya Hispania, La Liga inayoonyeshwa moja kwa moja na Azam TV, zinaweza kuahirishwa wikiendi hii kwa sababu ya hali ya joto kali, amesema Rais wa Ligi ya Soka Hispania (LFP), Javier Tebas.
    Joto limekuwa kali sana kiasi cha kufikia nyuzi 40 na kufanya mechi hususan zile za muda wa mchana zichezwe zitakazozikutanisha Celta Vigo vs Atletico Madrid na Real Madrid vs Osasuna kuwa ngumu kuchezeka.
    "Ikiwa kiwango cha joto kitafikia nyuzi 40 kwa mechi za wikiendi, baadhi ya mechi za La Liga zinaweza kuahirishwa,' alisema Tebas.


    Rais wa Ligi ya Hispania, Javier Tebas amesema Ligi haiwezi kuchezwa kwenye nyuzi joto 37

    "Huwezi kucheza mechi katika joto la nyuzi 36, 37 au 38. Tumejadili hali ya joto, siyo kwa sababu ya mechi za wikiendi hii, lakini kwa sababu ya mechi za raundi zilizotangulia. 
    Real Madrid walicheza mechi yao ya mwisho dhidi ya Celta Agosti 27 kwenye kiwango cha nyuzi joto 32,". 
    Tebas alisema kwamba Ligi itaangalia uwezekano wa kuchelewesha baadhi ya mechi, ingawa imeripotiwa kuna joto kali hata wakati usiku.
    Kiwano cha joto kinatarajiwa kuwa kati ya nyuzi 30 kwa wikiendi hii kote Hispania wakati wa usiku.
    Tebas amesema marefa walishauri wachezaji kupewa mapumziko mengi ya kunywa maji wakati wa mechi ili kukabiliana na hali hiyo. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JOTO KALI LAVURUGA LA LIGA, MECHI KUAHIRISHWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top