• HABARI MPYA

  Saturday, September 03, 2016

  HUKUMU YA KESSY YAPIGWA KALENDA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji iimeahirisha kikao chake kilichokuwa kikae kesho Jumapili Septemba 4, 2016 kutoa hukumu ya shauri la mchezaji Hassan Ramadhan Kessy anayedaiwa na Klabu ya Simba kuvunja mkataba kwa kuanza kufanya mazoezi na klabu ya Yanga SC sambamba na kusajili katika timu hiyo ya Mtaa wa Jangwani, Dar es Salaam kabla ya mkataba wake kufika mwisho Juni 15, 2016.
  Simba imelalamika mbele ya kamati hiyo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwa, mchezaji Hassan Kessy alivunja taratibu hizo akiwa ndani ya mkataba wa klabu hiyo yenye mashakani yake Barabara ya Msimbazi jijini Dar es Salaam.
  Hassan Kessy (kushoto) hukumu yake haitasomwa kesho kama ilivyopangwa awali

  Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati hiyo, shauri hilo lilisikilizwa baadaye mwezi huu katika tarehe itakayopangwa hapo baadaye. Sababu za kuahirisha kikao hicho ni kutotimia kwa akidi ya wajumbe wa kamati nzima. Akidi ni lazima wajumbe zaidi ya watatu wathibitishe kushiriki.
  Ilikuwa  isikiliwe kesho baada ya kushindikana kusikilizwa kwa shauri jingine linalohusu Klabu Simba ikiilalamikia Klabu Yanga SC, kuingia mkataba na mchezaji Hassan Ramadhani Kessy wakati bado ana mkataba na klabu Simba.
  Shauri la Simba dhidi ya Yanga lilishindika kusikilizwa kwa sababu Yanga hawakutokea mbele ya kamati hiyo wakati wa kusikiliza shauri hilo, hivyo kamati itaiandikia barua Young Africans kukumbushwa kuhudhuria kwenye kesi hiyo Jumapili ijayo kabla ya kutolewa uamuzi. Kama hawakutokea tena, shauri hilo litasikilizwa upande mmoja na kutolewa uamuzi upande mmoja. Kadhalika mashauri mengine yatakayosikilizwa hapo baadaye ni pamoja na yale ambayo wahusika walipewa nafasi ya kuyamaliza nje ya kamati lakini wakashindwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HUKUMU YA KESSY YAPIGWA KALENDA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top