• HABARI MPYA

  Sunday, September 04, 2016

  GUARDIOLA AMTEMA YAYA TOURE KIKOSI CHA LIGI YA MABINGWA MAN CITY

  KOCHA Pep Guardiola amemmaliza Yaya Toure kwa kutomjumuisha kwenye kikosi cha Ligi ya Mabingwa Ulaya, kwa mujibu wa wakala wake.
  Mkongwe huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 33 hajaichezea City katika mechi yoyote ya Ligi Kuu ya England baada ya mechi tatu za awali chini ya kocha mpya, Guardiola.
  Na pigo lingine kwa kiungo huyo wa zamani wa Barcelona aliyebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake Man City - atalazimika kukubali kutocheza mechi za Kundi Group C dhidi ya wapinzani Barcelona, Borussia Monchengladbach na Celtic.
  Wakala wa Toure, Dimitri Seluk, amesema kwamba shinikizo lipo kwa Guardiola sasa kushinda taji la mashindano hayo - na hiyo itamuondoka Uwanja wa Etihad mteja wake baada ya msimu.   
  "Huu ni uamuzi wa Pep na lazima tuuheshimu. Ikiwa ataipa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya Man City msimu huu nitasafiri hadi England na kusema kwenye Televisheni kwamba Pep Guardiola ni kocha bora duniani,".
  "Lakini ikiwa City haitoshinda Ligi ya Mabingwa natumai kwamba Pep atalazimika kukiri alikosea kumtema mchezaji mkubwa kama Yaya. Lakini nachoweza kukuambia ni kwamba Yaya atamaliza msimu City. Hataondoka January. Anatumai atapata nafasi ya kurudi kwenye kikosi,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GUARDIOLA AMTEMA YAYA TOURE KIKOSI CHA LIGI YA MABINGWA MAN CITY Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top