• HABARI MPYA

    Monday, September 05, 2016

    FUNGUA DIMBA AIRTEL RISING STARS TAIFA NI LINDI NA ARUSHA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU za soka za wasichana za Lindi na Arusha zimepangwa kukutana katika mechi ya fungua dimba ya mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Statrs ngazi ya taifa katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, jijini Dar es Salaam, Jumanne, Septemba 6, 2016.
    Mashindano hayo yanayojumuisha timu za wasichana na wavulana yatafunguliwa rasmi siku hiyo ya Jumanne mchana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda ambaye atashuhudia mechi ngumu ya wavulana kati ya Mwanza na Ilala.
    Timu nyingine zinazoshiriki katika michuano hiyo yenye lengo la kuibua vipaji ni Temeke, Kinondoni, Morogoro, Arusha, Mbeya, Lindi na Zanzibar. Tayari timu zimeshawasili na kupiga kambi katika shule ya Filbert Bayi iliyoko Kibaha.

    Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matinde akiongea wakati wa kuchezesha droo ya fainali za taifa ya michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars. Kushoto ni Mkurungenzi wa maendeleo ya soka la wanawake TFF Amina Karuma na katikati Mkurugenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi.

    Akizungumza wakati wa hafla ya kupanga makundi iliyofanyika katika ofisi za shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF), Mkurungenzi wa Ufundi Mwalimu Salum Madadi alisema kuwa maandalizi yote ya mashindano hayo ngazi ya taifa yamekamilika.
    Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na mkurengenzi wa maendeleo ya soka la wanawake nchini Bi Amina Karuma ambaye aliyaelezea mashindano ya Airtel Rising Stars kuwa ni chemchem ya wanasoka chipukizi wasichana kwa wavulana.
    “Mashindano ya Airtel Rising Stars yametusaidia kupata wachezaji wenye vipaji vya ajabu ambao wanaunda timu za Serengeti Boys na timu ya taifa ya wanawake yaani Twiga Stars”, alisema na kuwashukuru Airtel Tanzania kwa kuendelea kudhamini mashindano hayo.
    Kwa upande wake, Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde alisema kuwa kampuni yake inajivunia kuweza kutoa mchango katika soka la Tanzania. “Airtel Rising Stars imekuwa chanzo cha kutumainiwa kwa klabu na timu za Taifa kupata vijana chipukizi wenye vipaji. Tunaona fahari kuweza kupata fursa ya kudhamini soka nchini Tanzania“alisema Matinde. 
    Michuano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa inatarajia kufikia tamati siku ya Jumapili, Septemba 11, 2016 ambapo bingwa kwa upande wa wasichana na wavulana watapatikana na kukanidhiwa vikombe vya ubingwa.
    Vilevile TFF itatangaza wachezaji nyota kwa wasichana na wavulana wataochaguliwa kuunda timu ya Airtel Rising Stars mwaka 2016.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FUNGUA DIMBA AIRTEL RISING STARS TAIFA NI LINDI NA ARUSHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top