• HABARI MPYA

  Saturday, September 17, 2016

  BOSSOU NJE TENA NA LEO YANGA IKIIVAA MWADUI KAMBARAGE

  Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA
  BEKI hodari Mtogo, Vincent Bossou ataendelea kuwa nje ya kikosi cha Yanga SC katika mechi ya tatu mfululizo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Bossou mwenye asili ya Ivory Coast, hakuwepo wakati Yanga inatoa sare ya 0-0 na Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara na ikishinda 3-0 dhidi ya Maji Maji Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Lakini kukosa kwake mechi mbili zilizopita, ilielezwa ni kwa sababu alichelewa kurejea baada ya kuruhusiwa kwenda kuichezea Togo katika mechi ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika. 
  Vincent Bossou hajapangwa katika mchezo wa leo kwa sababu ni majeruhi

  Pamoja na kwamba yuko nchini tangu wiki iliyopita, lakini katika mchezo wa leo dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga Bossou hajapangwa kwa sababu ni majeruhi.
  Kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm amewaanzisha pamoja beki mpya, Andew Vincent Chikupe ‘Dante’ na Kevin Yondan.
  Kwa ujumla kikosi kilichopangwa na Pluijm leo ni; Ally Mustafa ‘Barthez’,  Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Andrew Vicent, Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Thabani Kamussoko, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Deus Kaseke.
  Katika benchi watakuwapo Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Mahadhi, Deo Munishi ‘Dida’, Oscar Joshua, Haruna Niyonzima, Obrey Chirwa na Yussuf Mhilu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BOSSOU NJE TENA NA LEO YANGA IKIIVAA MWADUI KAMBARAGE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top