• HABARI MPYA

  Monday, September 05, 2016

  BOSSOU AIPELEKA TOGO AFCON 2017 GABON

  TIMU ya taifa ya Togo imefuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Djibouti usiku wa jana Uwanja wa Kegue mjini Lome.
  Mabao ya The Sparrow Hawks yalifungwa na beki wa Yanga ya Tanzania Vincent Bossou, Mathieu Dossevi, Fo-Doh Laba na Komlan Agbegniadan mawili na Togo inamaliza nafasi ya pili kwenye Kundi A hivyo kufuzu Afcon ya kwanza tangu mwaka 2013, baada ya Tunisia iliyoifunga Liberia 4-1 na kumaliza kileleni.
  Timu 16 kwa ujumla ambazo zitashiriki michuano hiyo mwakani Gabon mbali na wenyeji hao, nyingine ni Algeria, Burkina Faso, Cameroon, Ivory Coast, DRC, Misri, Ghana, Guinea Bissau, Mali, Morocco, Senegal, Togo, Tunisia, Uganda na Zimbabwe.
  Uganda iliyomaliza nafasi ya pili Kundi D kwa pointi zake 13, na Togo, ya pili Kundi A kwa pointi zake 11 wamefuzu kama washindi wa pili bora.
  Guinea-Bissau itakuwa nchi pekee inayoshiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza kabisa, wakati Senegal imekuwa timu pekee iliyoshinda mechi zote sita za kundi lake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BOSSOU AIPELEKA TOGO AFCON 2017 GABON Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top