• HABARI MPYA

  Thursday, September 08, 2016

  BECHEM UNITED WATWAA UBINGWA WA KOMBE LA FA GHANA

  KWA mara ya kwanza katika hisrtoria yao, Bechem United imetwaa ubingwa wa Kombe la la Chama cha Soka Ghana baada ya kuifunga Okwawu United 2-1 katika fainali mwishoni mwa wiki, Jumapili ya Septemba 4 mjini Cape Coast.
  Yaw Arnol alifunga mabao mawili kuipa ushindi huo timu hiyo ya Ligi Kuu ya Ghana, huku Akoto Danso akiwafungia Okwawu bao la kufutia machozi.
  Baada ya kutofungana kipindi cha kwanza, Arnol aliifungia Bechem bao la kwanza dakika ya 55 kwa shuti kali.
  Okwawu, mabingwa wa michuano hiyo mwaka 1986, wakasawazisha bao hilo dakika ya 63 wakati Danso alipomalizia krosi ya Maclin Ampadu.
  Arnol akaifungia bao la ushindi Bechem mwishoni mwa mchezo akimalizia pasi ya Abednago Tetteh.
  Kwa matokeo hayo, Bechem itaiwakilisha Ghana kwenye Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, hiyo ikiwa mara yao ya kwanza kucheza michuano ya Afrika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BECHEM UNITED WATWAA UBINGWA WA KOMBE LA FA GHANA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top