• HABARI MPYA

  Thursday, September 15, 2016

  AKINA SAMATTA WAPIGWA 3-2 MECHI YA KWANZA YA MAKUNDI EUROPA LEAGUE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KRC Genk imeanza vibaya hatua ya makundi ya Europa League baada ya kufungwa mabao 3-2 na wenyeji Rapid Viena katika mchezo wa Kunfi F Uwanja wa Allianz, Viena, Austria.
  Hicho kinakuwa kipigo cha pili mfululizo kwa timu hyo ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta baada ya mwishoni mwa wiki kufungwa mabao 2-0 na Standard Liege katika Ligi ya Ubelgiji Jumapili Uwanja wa Maurice Dufrasne mjini Liege.
  Mabao ya Genk yamefungwa na Leon Bailey yote, la kwanza dakika ya 29 na la pili dakika ya 90 kwa penalti.
  Mbwana Samatta akipambana katika mchezo wa leo mjini Viena

  Mabao ya wenyeji, Rapid Viena yamefungwa na Stefan Schwab dakika ya 51, Joelinton Cassio Apolinario de Lira maarufu tu kama Joelinton dakika ya 59 na Omar Colley aliyejifunga dakika ya 60.
  Mchezo mwingine wa kundi hilo, wenyeji Sassuolo wameshinda 3-0 dhidi ya Athletic Athletic Bilbao ya Hispania Uwanja wa Citta del Tricolore, mabao ya Pol Lirola dakika ya 60, Gregoire Defrel dakika ya 75 na Matteo Politano dakika ya 82.
  Tangu amejiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, Samatta amecheza jumla ya mechi 25 za mashindano yote, 18 msimu uliopita na saba msimu huu, akifunga mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita.
  Katika mechi hizo, ni 14 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na tatu msimu huu, wakati 11 alitokea benchi nane msimu uliopita na tatu msimu huu – na mechi tisa hakumaliza akitolewa, sita msimu uliopita na tatu msimu huu.
  Kikosi cha Rapid Wien kilikuwa; Strebinger, Schösswendter, Schrammel, Schwab, Schaub, Dibon, Szanto/Hofmann dk61, Pavelic Traustason/Murg dk79 Mocinic na Joelinton/Kvilitaia dk86.
  KRC Genk : Bizot, Walsh, Dewaest, Colley, Uronen, Heynen/Susic dk78, Ndidi, Pozuelo, Bailey, Buffalo/Trossard dk64 na Samatta/Karelis dk78.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AKINA SAMATTA WAPIGWA 3-2 MECHI YA KWANZA YA MAKUNDI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top