• HABARI MPYA

  Tuesday, August 02, 2016

  SERENGETI BOYS YAITAFUNA 2-0 MADAGASCAR, KESHO YAENDA SAUZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa chini ya miaka 17, Serengeti Boys imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya leo wenyeji, ya Madagascar mjini Antananarivo leo.
  Katika mchezo huo wa marudiano baina ya timu hizo baada ya juzi kutoka ware ya bila kufungana, mabao ya Serengeti Boys yamefungwa na Cyprian Mtesingwa dakika 77 na Kelvin Nashon dakika ya 86.
  Serengeti Boys ilikuwa imeweka kambi mjini Antananarivo, Madagascar tangu wiki iliyopita kujiandaa na kucheza dhidi ya Afrika Kusini kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Jumapili wiki hii na kesho inaondoka.
  Serengeti Boys inakwenda Afrika Kusini tayari kwa mchezo wa kwanza Jumapili, kabla ya timu hizo kurudiana Agosti 21, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi, Dar es Salaam.


  Nyota walioko kambini ni pamoja na makipa, Ramadhani Awm Kabwili, Kelvin Deogratius Kayego na Samwel Edward Brazio wakati mabeki wako Kibwana Ally Shomari, Nickson Clement Kibabage, Israel Patrick Mwenda, Dickson Nickson Job, Ally Hussein Msengi, Issa Abdi Makamba na Enrick Vitalis Nkosi.
  Viungo ni Kelvin Nashon Naftal, Ally Hamisi Ng’anzi, Asadi Ali Juma Ali, Syprian Benedictor Mtesigwa, Ibrahim Abdallah Ali, Shaban Zuberi Ada huku washambuliaji wakiwa ni Mohammed Abdallah Rashid, Yohana Oscar Mkomola na Muhsin Malima Makame.
  Serengeti Boys inakwenda kucheza na Afrika Kusini baada ya kuwatoa Shelisheli kwa jumla ya mabao 9-0 katika mechi zake mbili za kimataifa. Mshindi wa jumla kati ya Serengeti Boys na Afrika Kusini, atacheza na timu mshindi kati ya Namibia na Congo-Brazaville.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAITAFUNA 2-0 MADAGASCAR, KESHO YAENDA SAUZI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top